SHARE

Matajiri wa Ufaransa, Paris Saint Germain (PSG), imeongeza kasi ya kumsajili kinara wa mabao wa Liverpool, Mohamed Salah katika usajili wa majira ya kiangazi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu akiwa amefunga mabao 29.

Salah mwenye miaka 29 alijiunga na Liverpool kutoka AS Roma ya Italia katika usajili wa majira ya kiangazi msimu uliopita.

Pia, amefunga jumla ya mabao 38, akitoa pasi za mwisho mara 13 katika mashindano tofauti msimu huu.

PSG inasaka mfungaji hodari wa mabao kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji nguli Zlatan Ibrahimovic anayecheza Los Angeles Galaxy ya Marekani.

Taarifa ya klabu hiyo imekuja wakati mchezaji huyo akiwa na anajiandaa na mchezo mgumu wa robo fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City kwenye Uwanja wa Etihad kesho.

Man City itakuwa nyumbani katika mchezo huo ikiwa na kibarua cha kurudisha mabao matatu iliyofungwa mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Anfield.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here