SHARE

Rais wa Barcelona Josep Bartomeu ameomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya timu hiyo kutupwa nje katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Barcelona iliyokuwa ikipewa nafasi ya kusonga mbele, iliondolewa na AS Roma ya Italia baada ya juzi usiku kuchapwa mabao 3-0 ugenini.

AS Roma imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini licha ya timu hizo kutoka sare ya jumla ya mabao 4-4.

Mbali na kutupwa nje, kibarua cha kocha Ernesto Valverde kinaweza kuoya nyasi kutokana na matokeo hayo ambayo hayakutarajiwa na mashabiki wa soka.

Kigogo huyo alisema amepokea kwa masikitiko matokeo hayo na hana njia nyingine zaidi ya kuwaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo ya Noy Camp.

“Naomba radhi sana. Roma walikuwa katika kiwango bora uwanjani na walikuwa sahihi kusonga mbele. Vijana walipambana lakini hali imekuwa tofauti na matarajio,”alisema Rais huyo.

Rais huyo alisema matokeo ya juzi usiku yanaiweka njia panda timu hiyo, lakini ana amini wachezaji watarejea katika ubora wake muda mfupi ujao kwa ajili ya mashindano mengine.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here