SHARE

Klabu ya AS Roma imetoa kali ya mwaka baada ya kuchapisha tiketi ya nusu fainali Ligi Mabingwa kuwa watacheza na Liverpool kabla ya kupangwa kwa ratiba mechi hiyo jana mchana.

Miamba hiyo ya Italia wamefanikiwa kutinga kwa nusu fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo baada ya kuiondoa Barcelona katika robo fainali.

Mafanikio hayo yamewafanya kuchapisha tiketi na kuwataka mashabiki wake wanunua katika mchezo wao wa nyumbani dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp.

Makosa hayo yaliyofanywa katika tovuti ya klabu hiyo yaliondolewa haraka baadaye, lakini tayari baadhi ya mashabiki walikuwa wamefanikiwa kupiga picha ‘screenshot’ tiketi hiyo inayoonyesha mechi hiyo itachezwa Mei 2.

Ratiba ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa itapangwa leo Ijumaa mchana huu Uswisi.

Timu nyingine zilizoingia kucheza hatua hiyo ni pamoja na mabingwa watetezi Real Madrid na vigogo wa Ujerumani, Bayern Munich wote wanasubiri ratiba hiyo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here