SHARE

Kocha wa Mbao, Ettiene Ndayiragije na Charles Mkwasa ametajwa kuwa ndiyo makocha pekee watakaoweza kuituliza Yanga katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondoka George Lwandamina.

Yanga imepata pigo hivi karibuni baada ya kocha Lwandamina kuondoka kimyakimya na kujiunga na klabu yake ya zamani za Zesco United, uamuzi ambao unalazimisha uongozi wa mabingwa hao kuanza kutafuta kocha mwingine wa kusaidiana na Shadrack Nsajigwa.

Lwandamina anaondoka katika kipindi ambacho Yanga ipo kwenye vita kali ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba pamoja na kuhakikisha wanalinda ushindi wao dhidi Weolayitta Dicha ya Ethiopia ili kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kutokana na hali hiyo mashabiki wa Yanga wanaamini Katibu Mkuu Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha na Mrundi Ndayiragije ndiyo watu sahihi wa kuibeba kutokana na uwezo wao wa kuweza kuendana na kasi ya sasa.

Katibu wa Mashabiki tawi la Mwanza Mjini, Mhando Madega alisema kwa sasa Yanga inapaswa kujipanga upya ni bora Mkwasa apewe kazi ya kuinoa kwani ana uwezo mkubwa.

“Tumesikitika kuondoka kwa Lwandamina, alikuwa mvumilivu, lazima uongozi ujipange kivingine na washauri kama uwezekano upo wampe Mkwasa mikoba aongoze timu,” alisema Madega.

Naye Khamis Maluli alisema Ndayiragije anafaa kupewa timu kwa kipindi hiki ili kuinusuru Yanga katika mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu na kushiriki vyema mashindano ya Kimataifa.

Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa Ndayiragije huenda akatua Yanga kurithi mikoba ya Lwandamina, baada ya mambo kutoenda sawa ndani ya Mbao.

Katika mchezo wa juzi Jumatano kocha huyo Mrundi haukaa katika benchi timu yake iliposhinda 2-1 dhidi ya Njombe, huku jukumu likisimamiwa na Kocha Msaidizi, Ahmad Ally na Meneja wa timu, Faraji Muya ikielezwa kuwa sababu ya kutokufika uwanjani hapo ni matatizo ya kiafya.

Tayari uongozi wa Mbao umetangaza kumnasa aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Novatus Fulgence. Mwenyekiti wa timu hiyo, Solly Njashi alisema waongeze nguvu ili kuinusuru timu kushuka daraja na kwamba ujio wa kocha huyo si kwamba Ndayiragije amefukuzwa kazi, bali watashirikiana wote.

Singida waipa nuksi Yanga

Sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida United juzi imeifanya Yanga kuifikia rekodi iliyoweka msimu wa 2013/2014 lakini huenda ikaipa mkosi kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kama ilivyotokea miaka minne iliyopita.

Kabla ya matokeo hayo dhidi ya Singida United, idadi kubwa ya sare ambazo Yanga ilizipata kwenye Ligi Kuu kwa msimu mmoja ilikuwa ni nane (8) ambazo timu hiyo ilizipata katika msimu huo wa 2013/2014 ambapo matokeo hayo yalipatikana kwenye mechi dhidi ya timu za Coastal Union, Mbeya City, Prisons, Simba, Azam na Mtibwa.

Matokeo hayo ya juzi dhidi ya Singida United, yameifanya Yanga ifikishe jumla ya sare nane katika michezo 22 iliyocheza kwenye Ligi Kuu msimu huu na kufikia rekodi ya msimu huo wa 2013/2014 ambapo ilikuwa ndio idadi kubwa ya sare kuzipata ndani ya msimu mmoja.

Sare hizo nane ambazo Yanga imezipata msimu huu ni dhidi ya timu za Lipuli, Simba, Mtibwa, Mwadui, Majimaji, Prisons, na Singida United ambayo imetoka nayo sare nyumbani na ugenini.

K

atika msimu wa 2013/2014 Yanga iliweka rekodi hiyo ya kupata idadi sare nyingi lakini, haikufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ambao ulitwalichukuliwa na Azam FC.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here