SHARE

SIMBA inafurahia huduma bora ya kiraka wake, Mghana Asante Kwasi iliyemnunua kutoka Lipuli FC ya Iringa, lakini huko unadhani Yanga wenye Ibrahim Ajibu wanafurahia hilo.

Tangu ametua klabuni hapo, Kwasi amekuwa moto kwelikweli huku akisaidia Simba kupata matokeo muhimu kwa kupachika mabao licha ya kuwa ni beki.

Kwasi, ambaye amekuwa akicheza nafasi ya ulinzi tangu ameanza msimu, ambapo mzunguko wa kwanza alicheza beki wa kati akiwa na Lipuli na beki wa kushoto kwenye kikosi cha Simba.

Lakini, sasa pamoja na kucheza nafasi hiyo amekuwa hakamatiki kwenye kutupia mabao na kukimbizana na mastaa wanaocheza nafasi za ushambuliaji na viungo. Iko hivi. Nyota wa Yanga Ibrahim Ajib ana mabao saba mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara sawa na Shiza Kichuya wa Simba, idadi ambayo tayari Kwasi ameifikia.

Kwasi anazidiwa mabao 11 na kinara wa safu hiyo kwenye msimamo wa ligi, Emmanuel Okwi ambaye pia ni wa Simba aliyefunga mabao 18.

Mbali na Okwi wengine wanaomzidi ni John Bocco ‘Adebayor’ ambaye pia ni wa Simba ana 12, Mzambia Obrey Chirwa wa Yanga ana 12, Habib Kyombo wa Mbao ana tisa sawa na Eliud Ambokile wa Mbeya City, Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons na Marcel Boniventure wa Majimaji wana manane.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here