SHARE

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameondoka jana Aprili 15, 2018 kwenda jijini London nchini Uingereza kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM).

Mkutano huo utafanyika kuanza leo, Aprili 16 hadi 20 na utafunguliwa na Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza ukiwa na kaulimbiu inayosema, “Kuelekea mustakabali wa pamoja” na utaongozwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May atakayekuwa mwenyekiti.

Taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Makamu wa Rais imesema majadiliano ya mkutano huo yatajikita kwenye maeneo manne makuu ya kipaumbele ambayo yatajadili namna ambavyo Jumuiya ya Madola inaweza kufikia mustakabali wenye ustawi zaidi; mustakabali endelevu zaidi; mustakabali wenye haki zaidi na mustakabali wenye usawa zaidi.

“Mijadala katika maeneo hayo ya kipaumbele itahusisha masuala mbalimbali ikiwemo kukuza zaidi biashara na uwekezaji baina ya nchi za Jumuiya ya Madola kwa manufaa ya nchi wanachama na Jumuiya nzima.

Pia, kukuza na kuendeleza misingi ya demokrasia, ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu pamoja pamoja na masuala ya uhalifu wa kimataifa kama vile ugaidi, uhalifu wa kimtandao na usafirishaji wa binadamu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Makamu wa Rais amembana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka wizara hiyo ambapo msafara huo unatarajia kurejea nchini Aprili 22.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here