SHARE

Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Tanzania, Getrude Lwakatare ametunukiwa tuzo ya heshima na utumishi bora wa kiroho na jamii na Shirika la Umoja wa Maaskofu na Wachungaji Ulimwenguni.

Mchungaji Lwakatare anakuwa wa kwanza kukabidhiwa tuzo hiyo kwa Afrika Mashariki na amekabidhiwa jana Aprili 15, 2018 na Askofu mkuu shirika hilo kwa Afrika, Profesa Leonard Kawas kutoka Nigeria.

Profesa Kawas asema tuzo hiyo imetolewa na Rais wa shirika hilo, Steven More na anakuwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa.

“Mchungaji Lwakatare ni mwanamke aliyebeba maono, ni mtu wa kukata na shoka asiyekata tamaa Mungu akubariki sana. Umefanya kazi kubwa sana za kiroho na kuisadia jamii,” amesema Profesa Kawas.

Amesema Mchungaji Lwakatare amekuwa mtu wa kujituma na amefanya kazi kubwa hasa katika sekta ya elimu kupitia shule anazozimiliki sanjari na kutoa huduma za kiroho kupitia kanisa lake.

Amesema tuzo hiyo imeshatolewa Uingereza, Amerika na Afrika na hakukuwa siasa na Mchungaji Lwakatare hakuomba bali waliangalia utendaji kazi wake.

Kwa upande wake, Mchungaji Lwakatare ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu (CCM) amemshukuru Mungu kwa tuzo hiyo na hakutarajia kama atatunukiwa.

“Kumbe watu wa nje wanaangalia unachofanya, nilijua Watanzania tu. Namshukuru Mungu wa nje wameona ninanchokifanya kuanzia kwenye jamii hadi katika huduma za kiroho,”amesema Mchungaji Lwakatare.

Mchungaji Lwakatare amesisitiza kuwa sifa za pekee zimwendee Mungu na kuwataka Watanzania kutenda mambo mema kwa watu wote bila kuwabagua na ataliombea shirika hilo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here