SHARE

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa Majaji 10 wa Mahakama Kuu ili kujaza nafasi za majaji waliostaafu.

Mbali na majaji, Rais amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali kwa lengo la kuhakikisha ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali inafanya kazi kikamilifu.

Taarifa iliyotolewa jana Aprili 15, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa imewataja walioteuliwa kuwa ni Dk Evaristo Lungopa aliyeteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anachukua nafasi ya Paul Ngwebe ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Edson Makallo ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka; Dk Julius Mashamba ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali huku Dk Ally Possi akiteuliwa kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Majaji wengine walioteuliwa ni Elvin Claud Mgeta, Elinaza Benjamin Luvanda, Yose Joseph Mlyambina, Immaculata Banzi, Mustafa Siyani, Agnes Zephania Mgeyekwa, Stephen Murimi Magoiga, Thadeo Mwenampazi pamoja na Butamo Philip.

Kabla ya uteuzi huo, Butamo Philip alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here