SHARE

Jeshi la Polisi limemkamata msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa tuhuma za kusambaza picha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amethibitisha hilo bungeni, Dodoma leo baada ya Mbunge kuibua suala mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Waziri amemtaja msanii Faustina Charles ‘Nandy’ naye yupo mikononi mwa Polisi kwa sababu ambazo zinahusishwa na ukiukwaji wa maadili.

Awali, Naibu wake Juliana Shonza aliwakumbusha wasanii kuhakikisha kazi zao zinakaguliwa kabla ya kusambazwa.

Waziri Mwakyembe ameliambia Bunge kuwa mtandao si sehemu ya kubeba kila kitu


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here