SHARE

MAMA wa bibi harusi, Amina Rikesh aliyefunga ndoa na mwanamuzi wa Bongo Freva Ali Kiba, ametoa la moyoni na kusema, hakujua kama msanii huyo mkubwa Afrika Mashariki ndiye anamwoa mtoto wake.

Mama huyo anayeitwa, Asma Said anasema, hakujua kama anayemwoa ni Ali Kiba na alijua ni kijana tu kutoka Tanzania.

“Kijana ametoka Tanzania na kuja kuoa Kenya mimi sikujua kama mtoto wangu ataolewa na Ali Kiba lakini Mungu ndio aliyepanga,” anasema mwanamke huyo.

Ali Kiba alifunga ndoa katika Msikiti wa Ummul Kulthum uliopo eneo la Kizingo jijini Mombasa, Kenya. Msikiti huo umejengwa na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho na baadaye kufuatiwa  na sherehe kubwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Mombasa.

Msanii huyo anayetamba na wimbo wake wa Seduce Me, aliingia Kenya jana Jumatano na kukaa katika hoteli ya English Point Marina iliyo karibu na nyumba ya bibi harusi maeneo ya Kongowea.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here