SHARE

Wasanii mbalimbali nchini wameonyesha masikitiko kupitia mitandao yao ya kijamii, baada ya kupata taarifa za kifo cha msanii mwenzao, anayepamba video za muziki, (Video Queen) Agnes Gerald maarufu Masogange.

Wakili wake, Reuben Simwanza amezungumza na MCL Digital na kuthibitisha kuwa Masogange amefariki leo.

Aslay Isihaka ameweka picha ya Masongange na kuandika, “Dah mbele yako nyuma yetu sister, safari yetu moja innalillah wainnailah raajiun,”

Huku Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnum’ akiweka picha ya mishumaa na maneno, “Rest in paradise Agnes.”

Rajab Kahali ‘Harmonize’ ameweka picha ya Masongange na kusema, “God’s plan R.I.P. Aggy.

Naye Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameweka picha tatu tofauti za Masogange na kuzungumzia kifo hicho akianza kwa kusema;

“Nimepokea taarifa ya kifo chako kwa mshtuko mkubwa sana. Masogange amka mama Masogange. Staki kuamini.”

Mcheza filamu, Wema Sepetu ameweka picha ya Masongange ikiambatana na maneno, “Innah lillah wa innah illah rajiun… Dah…!


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here