SHARE

WANAFUNZI wa kike katika shule za msingi mkoani Rukwa wanafanya ngono zembe wakiwa na umri kati ya miaka sita na 13, baadhi yao wamekatiza masomo na ndoto zao baada ya kupata ujauzito, imebainishwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amebainisha hayo wakati akizindua utoaji wa chanjo mpya ya kinga dhidi ya kirusi kinachosababisha saratani ya mlango wa kizazi (HPV) uliofanyika katika Shule ya Sekondari Mazwi juzi katika Manispaa ya Sumbawanga.

Chanjo hiyo ambayo inatolewa kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 inatarajiwa kunufaisha wasichana 26,234 mkoani Rukwa.

“Wanafunzi wa kike wanashiriki ngono wakiwa katika umri mdogo kabisa, takwimu zilizopo zinaonesha kuwa mkoani Rukwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wanafunzi 325 walipata ujauzito, idadi kubwa walikuwa wakisoma katika shule za sekondari ambao walifikia 288.

“Huku waliokuwa katika shule za msingi ni 37, wanafunzi wanaosoma katika shule za msingi ni wenye umri wa miaka sita hadi 13, kwa mantiki hii tayari wanashiriki ngono,” amesema.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here