SHARE

Huenda unajiuliza ni utaratibu gani ulitumika kumpa Diamond Platinumz kazi ya kushiriki wimbo maalumu wa Kombe la Dunia, jibu ni kwamba umahiri wake ulitumika kama kigezo.

Raia wa Afrika Kusini na mdau mkubwa wa burudani barani Afrika, Tim Horwood alipewa kazi ya kutafuta wanamuziki watano kuifanya kazi hiyo.

Alipofika ukanda wa Afrika Mashariki anasema hakuna jina jingine lililomjia katika orodha yake fupi zaidi ya Diamond.

Horwood anasema ni msanii aliyeimarisha himaya yake ukanda wa Afrika Mashariki hivyo haikuwa rahisi kumchagua mwingine.

Wasanii wengine waliopata shavu hilo ni Sami Dan wa Ethiopia; Lizha James wa Mozambique; Ykee Benda wa Uganda; na Casper Nyovest wa Afrika Kusini.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here