SHARE

UONGOZI wa klabu ya African Lyon inayojiandaa kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, upo kwenye mchakato wa kumleta kocha wa kigeni raia wa Ufaransa.

Mmiliki wa klabu hiyo, Rahim Kagenzi, bila kutaja jina, amesema yupo katika hatua nzuri za kumleta kocha mwenye Leseni A ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).

Alisema dhamira yao ni kuona timu hiyo inafanya vizuri msimu ujao, hivyo wameanza maandalizi ya mapema.

“Tunataka kufanya vizuri msimu ujao, tuwe timu ya ushindani tuonyeshe tofauti na misimu yote iliyotangulia, na ili tufanikiwe, lazima tuwe na maandalizi mazuri,” alisema Kagenzi.

Alisema pia wana mpango wa kuongeza wachezaji wengine kwenye kikosi chao ili kukiimarisha.

African Lyon kwa mara ya kwanza ilipanda Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 kabla ya misimu miwili baadaye kushuka.

Timu nyingine zilizopanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao ni pamoja na KMC, JKT Tanzania za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Biashara United (Mara) na Alliance Schools ya Mwanza.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here