SHARE

Makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amekabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya 1,457 akiwamo aliyekuwa mjumbe wa Baraza la vijana CUF Taifa, Salim Mussa Omar.

Dk Shein alikabidhi kadi hizo juzi katika mwendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na mabalozi wa CCM Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika Wilaya ya Amani, Unguja.

Baada ya kukabidhiwa kadi, Salim alisema uamuzi wa kujiunga na CCM umetoka ndani ya moyo wake wala hakushinikizwa.

Dk Shein alisema dhamira ya Serikali ni kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/20, ili Zanzibar iwe na miji bora na ya kisasa.

Naye naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdallah Juma Mabodi alisema ziara hiyo inatokana na matakwa ya sera za chama hicho zinazomtaka kila kiongozi kushuka ngazi za chini kuangalia utekelezaji wa ilani.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here