SHARE

Msanii wa filamu Steve Nyerere amefungukia na kueleza kuhusu tuhuma zinazodaiwa na wana ndugu wa marehemu Masogange wakiwemo wifi zake kwamba hawakupata taarifa kuhusu fedha ambazo zilichangwa na kamati ya wasanii, kwa ajili ya kumsaidia mtoto Sania wa marehemu Agnes Masogange.

Steve Nyerere  amesema malalamiko ya ndugu hao kuhusu kutopewa michango iliyokusanywa na wasanii katika mazishi ya marehemu Agnes Masogange wanayafanyia kazi

“Tulitangaza kwa umma pale Leders Club na baada ya hapo tuliwafata familia na kuwaambia fedha hii iliyobaki ni milioni mbili na laki moja kwa ajili ya mtoto, aidha tunamuwekea katika akaunti mtoto.”

Siku mbili zilizopita, mmoja wa ndugu wa Agnes Masogange, aliyejulikana kwa jina la Sada, alisikika katika kituo kimoja cha televisheni kuwa,hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa kamati iliyoundwa na wasanii, ambayo pia ilisimamia kwa kiasi kikubwa mazishi ya Agnes Masogange na wala hawajawasiliana nao.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here