SHARE

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema hawezi kutoa pole kwa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Emmanuel Masonga baada ya kuachiwa huru kutoka gerezani jana Mei 10, 2018 maana katika nyakati za Udikteta wapinzani wote ni wafungwa watarajiwa.

Zitto ameandika katika kurasa zake za mitandao ya kujamii baada ya Sugu na Mwenzake kuachiwa huru kutoka gereza la Ruanda lilopo mkoani Mbeya.

“Nafurahi kuwa Mbunge Mbeya Mjini Ndg. Joseph Mbilinyi (Sugu) na mdogo wangu Emmanuel Masonga wametoka Gerezani! siwapi pole, maana katika nyakati za Udikteta wapinzani wote ni wafungwa watarajiwa. Naamini kukaa kwao gerezani kumewaongezea zaidi ari ya kupambania Demokrasia pana ya Nchi yetu.Watawala mjue sasa kuwa vifungo vya Uonevu, kututishia Maisha na hata kutupiga risasi havita turudisha nyuma kwenye kupigania demokrasi ya nchi yetu.“ameandika Zitto Kabwe kwenye wake wa Facebook.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here