SHARE
Muonekano wa moja ya Jengo la darasa la Shule ya Msingi Kitomanga lililopo katika Halmashauri ya Lindi Vijijini Mkoani Lindi liliojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).

Mpango wa lipa kulingana na matokeo EP4R umechangia kupunguza ndoa za utotoni kwa wanafunzi wanaokaa mbali na shule kwa wilaya ya Ruanga mkoa wa Lindi.
Akiongea na timu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari na maafisa wa elimu mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Ruanga Herbert Ngonyani amesema kwa kipindi cha nyuma walipokea kesi za wanafunzi wa kike watano kupata mimba hali iliyopelekea kukatisha masomo yao wakiwa wadogo na kuongea idadi ya watu wasio na elimu ya kusoma na kuandika.
Amesema mradi huo wa EP4R umesaidia kuboresha na kujenga majengo ya vyumba vya madarasa, mabweni ,bwalo lakulia chakula pamoja na vyoo vya wanafunzi wenye ulemavu hali ambayo imeongeza morali kwa wanafunzi kuudhuria masomo yao kila siku na kufwata maadili wanayofundishwa na walimu wao.
Serikali kupitia wizara ya elimu,sayansi na tekinolojia ilipeleka zaidi ya shilingi Milioni 200 katika shule ya sekondari Ruanga kwaajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo kati ya Bilioni 2.8 zilizotolewa kwaajili ya zoezi hilo kwa mkoa wa Lindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here