SHARE

Kampeni ya Ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam imezidi kupamba moto ambapo baadhi ya ofisi ujenzi wake umekamilika kwa kiasi kikubwa tayari kwa kukabidhiwa.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi huo kwa baadhi ya shule, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema miongoni mwa shule zilizokamilika ni shule ya Kasulu Ilala, Shule ya Sekondari Makumbusho iliyojengwa kwa ufadhili wa ubalozi wa China waliojitolea kujenga shule tano kwenye wilaya zote za Dar es salaam.

RC Makonda amesema ndani ya ofisi hizo kutakuwa na Ofisi ya mwalimu mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi, ofisi ya walimu wa kawaida, ukumbi wa mikutano, chumba cha kuhifadhi mitihani, vifaa vya michezo, chumba cha muhasibu, chumba cha kubadili nguo, mapokezi, bafu, vyoo, ofisi ya karani huku zikisheheni samani za kisasa kama viti, Meza, Makabati, AC, Feni na TV.

Aidha RC Makonda amesema mbali na kujenga ofisi za walimu pia atahakikisha shule zote za mkoa wa Dar es salaam zinakuwa na umeme pamoja na maji ya kutosha ambapo amepata wadau watakaochimba visima 50 kwenye shule zenye uhitaji.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here