SHARE

KOCHA msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa ‘Fuso’ ameachana ramsi na klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika.

Nsajigwa aliyedumu Yanga kwa kipindi kirefu, anaachana na timu hiyo wakati ambapo matokeo ya timu hiyo hayaridhishi na sasa anafuata nyayo za aliyekuwa kocha wake mkuu George Lwandamina.

Kocha huyo aliyeichezea Yanga kwa mafanikio makubwa enzi za uchezaji wake, alikuwa nahodha wa kikosi hicho kabla ya kutundika daluga na kuamua kuwa kocha wa vijana kabla ya kupandishwa kuwa msaidizi wa aliyekuwa kocha wao Hans van Plujim anayeinoa Azam FC kwa sasa.

Nsajigwa aliingia katika mzizo na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wakimshinikiza kujiuzulu kufuatia matokeo mabovu ya timu hiyo katika msimu wa Ligi uliomalizika wa 2017-18.

Aidha kufuatia tuhuma za kuwa alikuwa haelewani na wachezaji, Nsajigwa amezikanusha na kusema kuwa hajawahi kuwa na mgogoro na wachezaji na waliishi kwa amani kipindi chake chote.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here