SHARE

Tabia ya kupiga picha binafsi maarufu kama ‘selfie’ imezua hisia nchini Italia baada ya kijana mmoja kukutwa akipiga picha hizo kwenye eneo ambalo mwanamke amegongwa na treni.

Kijana huyo ambaye alikuwepo eneo la ajali hiyo iliyotokea kituo cha treni cha Piacenza cha Kusini mwa Italia, alisogea hatua chache mbele na kuanza kupiga picha wakati mwanamke huyo akipewa huduma ya kwanza.

Askari aliyekuwa eneo hilo alimfuata kijana huyo na kumuamuru afute picha zote alizopiga kwenye eneo hilo.

Mashuhuda wengine waliokuwa katika eneo hilo walilaani kitendo alichofanya kijana huyo, huku Mpigapicha aliyekuwepo pia kusema kwamba “tumepoteza maadili kabisa.”


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here