SHARE

Uongozi wa Klabu ya Simba unatarajia kugawa Tuzo kwa wachezaji wake Jumatatu ya wiki ijayo katika Hoteli ya Kempiski jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo ni kwa ajili ya wachezaji wao waliofanya vizuri kwa kipindi cha msimu wa ligi kuu uliomalizika pamoja na michuano mingine ya Kimataifa ambapo wao walishiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Pia, zawadi hizo zimepewa jina la MO Simba Awards ambapo zitahusisha nafasi mbalimbali kama kipa bora, beki bora, kiungo bora na mshambuliaji bora.

Hata hivyo, Tuzo hizo zitatolewa ikiwa ni siku moja baada ya mashindano ya SportPesa yanayoendelea nchini Kenya yatakayohitimishwa Jumapili hii .

Simba inayonolewa na Kocha Pierre Lechantre ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ukiwa ni wa 19 tangu timu hiyo ianzishwe.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here