SHARE

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha msafara wa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Kheri James.

Ajali hiyo ilitokea jana eneo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu. Ilitokea muda mfupi baada ya msafara kuingia Meatu ukitokea wilayani Itilima.

Kamanda wa polisi mkoani Simiyu, Boniventure Mushongi alisema ajali ilitokea baada ya basi kuligonga kwa nyuma moja ya magari yaliyokuwa kwenye msafara huo.

Naye mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alimtaja aliyefariki dunia kuwa ni diwani wa Tindahuligi, Seleman Mahoga.

“Madiwani wengine wanne wamejeruhiwa na wamepelekwa katika Hospitali ya Mwandoya,” alisema Mtaka.

Majeruhi hao walitarajiwa kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here