SHARE

KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude amesema kuwa ‘moto’ watakaokuwa nao msimu ujao ‘hautazimwa kirahisi’ na timu yoyote watakayokutana nayo.

Mkude alisema kikosi cha Simba msimu ujao kitakuwa imara zaidi ya kilivyo sasa kutokana na benchi la ufundi kukiimarisha kwa kusajili wachezaji wenye ubora.

Kiungo huyo alisema pia wachezaji wapya waliotua kwenye kikosi chao wataongeza ushindani wa kuwania namba katika kikosi cha kwanza.

“Mimi naona tutakuwa imara zaidi, tutakuwa na wachezaji wengi wazuri na hata kwa upande wa makocha watakuwa na wigo mkubwa wa kuchagua kikosi,” alisema Mkude.

Aliongeza kuwa wapinzani wao watatakiwa kujituma ili wapate ushindi na wao wanaamini hakuna timu itakayoweza kuwasumbua katika msimu ujao.

“Sasa hivi kila timu ipo kwenye kipindi cha kujiimarisha kwa usajili, naamini ligi itakuwa na upinzani zaidi ya msimu uliopita,” aliongeza kiungo huyo.

Klabu hiyo juzi ilitangaza rasmi kuwasajili, Meddy Kagere, Deogratias Munishi ‘Dida’ na Pascal Wawa baada ya kukamilisha usajili wao.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here