SHARE

Baada ya kukosa mechi takribani tatu za Ligi Kuu Bara, imeelezwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (UTC) inayomhusu Kiungo Mzambia, Clatous Chama, tayari imeshawasili nchini.

ITC imemfanya Chama kukosa mechi tatu ambazo ni dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Ngao ya Jamii, dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City katika Ligi Kuu Bara.

Kiungo huyo fundi aliwasili nchini kujiunga na Simba baada ya mabosi wake kumalizana na Dynamo FC ambayo alikuwa akiichezea huko Zambia.

Ujio wa ITC hiyo utamfanya Chama sasa kuanza kazi take rasmi ndani ya wekundu wa Msimbazi akiungana na Deogratius Munish ‘Dida’ ambaye tayari naye ITC yake imeshawasili.

Chama ataanza kibarua chake cha kwanza kuichezea Simba dhidi ya Lipuli, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here