SHARE

Nahodha wa timu ya Taifa, ‘Mbwana Samatta’ amekuwa gumzo nchini Uganda zikiwa zimebaki siku chache kabla ya timu hizo kuteremka uwanjani kupepetana katika mchezo utakaochezwa keshokutwa Jumamosi.

Taifa Stars na Uganda zinatarajiwa kumenyana katika mchezo wa kufuzu Faianali za Afrika (Afcon), mchezo uliopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Namboole, mjini Kampala.

Wakati Taifa Stars inaondoka leo mchana kwenda Uganda, homa ya mchezo huo imewakumba wananchi wa nchi hiyo huku jina la Samatta likipamba vyombo vya habari.

Jana na leo, vyombo vya habari Uganda vimemtaja Samatta ni mshambuliaji hatari anayepaswa kupewa ulinzi mkali katika mchezo huo.

Mchezaji huyo amekuwa na kiwango bora katika kikosi cha KRC Genk ya Ubelgiji, akiwa ndiye kinara wa mabao katika mashindano mbalimbali yakiwemo ya Ulaya.

Mbali na Samatta, nyota wengine wanaocheza soka la kulipwa waliomo katika kikosi hicho ni Simon Msuva (Al Jadida, Morocco), Hassani Kessy (Nkana, Zambia), Thomas Ulimwengu (Al Hilal, Sudan) Rashid Mandawa (BDF XI, Botswana) na Abdi Banda (Baroka, Afrika kusini).


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here