SHARE

MSHAMBULIAJI wa Simba, Marcel Kaheza, amesema anapambana kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Mbelgiji Patrick Aussems.

Kaheza, ambaye alisajiliwa na Simba msimu huu akitokea Majimaji ya Songea, bado hajajihakikishia namba kwenye kikosi cha timu hiyo.

Akizungumza juzi baada ya mchezo wa kirafiki wa timu hiyo dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, Kaheza, alisema kwa sasa anapambana na kujituma ili apate namba kwenye kikosi cha kwanza.

Alisema amejipanga kutumia vema kila nafasi na dakika anazozipata uwanjani.

“Timu inaendelea vizuri… changamoto za namba zipo, lakini najituma na kupambana ili kupata nafasi ya kucheza na ndio maana najitahidi kufanya vizuri katia kila nafasi ninayopata ya kucheza,” alisema Kaheza.

Nyota huyo juzi alifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 4-2 walioupata dhidi ya AFC Leopards katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Taifa.

Simba kwa sasa wanajiandaa na michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya ligi hiyo kusimama kwa muda kupisha michezo ya kimataifa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here