SHARE

Chama cha Chadema kimeapa kulinda kura zake za uchaguzi wa Jimbo la Ukonga na kuonya ole wao watakao thubutu kupindisha matokeo ya uchaguzi huo, iwapo mgombea wake atakuwa ameshinda.

Viongozi waliokuwa wakimnadi mgombea wa chama hicho katika kata ya Mongolandege wamesema baada ya kupiga kura wataendelea ‘kukomaa’ kulinda kura mpaka kitakapoeleweka.

Akizungumza kwenye kampeni hizo, Katibu wa Chadema Wilaya ya Ilala, Gervas Lyenda alisema watalinda kura na hawatakubali kupokwa ushindi wao.

Lyenda aliwataka wananchi wa kata hiyo kutumia wembe uleule waliotumia kuinyoa CCM katika uchaguzi wa mwaka 2015 kumnyoa Waitara.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Chadema, Frederick Sumaye alisema ni kawaida siku ya kupiga kura kuona magari mengi ya polisi yakirandaranda mitaani kwa lengo la kuwataka kuwatisha wananchi, lakini akawataka kutoogopa na wajitokeze kupiga kura.

Alisema wananchi hawapaswi kuogopa kwa vile Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi kihalali licha kwamba chama tawala kimeendelea kutumia dola kawatisha wananchi.

Msangi akiomba kura kwa wananchi alisema hana fedha za kuwanunua, bali anachoweza kuwaahidi wakimchangua ni kuwaletea maendeleo.

“ Hata kama nitakuhonga elfu tano kisha ukanichagua nitakulingia…Sita wajibika,” alisema.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here