SHARE

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema hata yeye anaweza kuhama endapo chama chake cha CCM hakitakuwa na tija kwa wananchi kwani hatokuwa na sababu za kuendelea kukitumikia.

Bashe amefunguka hayo katika kampeni za kumnadi mgombea ubunge jimbo la Ukonga ambapo amedai kuwa zipo sababu za kwa nini aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo (Chadema), Mwita Waitara kuhama chama hicho na kujiunga CCM kwa kuwa ni haki ya kisheria.

Bashe amesema ipo hoja inayosemwa kwamba Waitara amenunuliwa, hilo si kweli na kwamba anamfahamu kiongozi huyo tangu wakiwa pamoja Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) hivyo kudai kuwa hoja hiyo ni dhaifu.

“Aliondoka mzee Augustine Mrema mwaka 1995, Maalim Seif naye akaondola hadi mzee wangu Lowassa alifanya hivyo, hatujawahi kutuhumu kama mtu amenunuliwa, yoyote anapoamua kuwatumikia wananchi anapanda basi, vyama vya siasa ni sawa na basi, ukiona basi hilo dereva, kondakta hamuelewani unaweza kushuka kwenye basi hilo”amesema Bashe.

Jumapili ya Septemba 16, ni siku ambayo utafanyika uchaguzi mdogo katika majimbo mawili la Monduli, Ukonga na kata nyingine 22 nchini. Katika siku hizo za lala salama hamasa na nguvu ya kampeni inazidi kuongezeka kwa kila upande, hasa vyama viwili vyenye ushindani mkubwa nchini CCM na Chadema.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here