SHARE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema anashangaa kwanini wananchi huchukua hatua ya kuchoma Kituo cha Polisi pindi inapodaiwa kuna mtuhumiwa amefia kituo cha polisi lakini hawachomi kitanda mtu anapofariki akifanya mapenzi.

Kauli hiyo ameitoa bungeni jijini Dodoma leo wakati akijibu swali la nyongeza za Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF), aliyetaka kujua kauli ya waziri kutokana na hatua ya watu kufia mahabusu wakidaiwa kuteswa na polisi.

“Katika siku za karibuni zimejitokeza tabia mbaya na ovu za wananchi kufia kwenye vituo vya polisi mahabusu wanapokuwa wanashikiliwa wanapata mateso ambayo husababisha vifo vyao, na hivi karibuni kuna baadhi ya jamii zimekataa maiti kwenda kuzizika kutokana na kufia ndani ya vituo vya polisi, mheshimiwa waziri unatoa kauli gani kali kukemea hatua hii ambayo inatia aibu nchi yetu ambayo ni ya haki na demokrasia,” ameuliza Khatibu.

Akijibu swali hilo, Lugola amesema mwananchi kufa anakufa wakati wowote, mahali popote na ndiyo maana sijui kwenye Quraan, kwenye Biblia Mhubiri 9:12 nenda kasome… ‘kifo ni mtego, kifo humnasa mtu wakati wowote mahali popote’. Kwa hiyo mwananchi anaweza akafa akiwa polisi, akiwa anafanya mapenzi, akiwa kwenye gari anasafiri anaweza akafia hata humu ndani ya bunge.

“Kwa hiyo isije ikachukuliwa kwamba aliyefia kituo cha polisi ni kwamba ameteswa, lakini ninakiri kwamba kumekuwa na matukio ambapo wananchi wanafia mikononi mwa polisi huwa tunafanya uchunguzi na pale inapobainika kwamba polisi wamehusika tumekuwa tukichukua hatua na ndiyo maana tumekuwa tukizuia wananchi kujichukulia sheria mikononi kwa kuchoma kituo cha polisi.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here