SHARE

MAWAZIRI wameunga mkono wazo la kujirekodi wanapojibu maswali ikiwa siku moja baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwataka kufanya hivyo.

Juzi, wakati wa kuhitimisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria MbalimbaliNa. 3 wa mwaka 2018, Spika Ndugai aliwataka mawaziri kwenda kisasa kwa kuitumia mitandao ya kijamii ikiwamo ‘You Tube’ kujirekodi pindi wanapojibu hoja mbalimbali bungeni kama wanavyofanya wabunge wa upinzani.

Wakizungumza na gazeti la Nipashe jana, baadhi ya mawaziri na naibu mawaziri walisema wazo hilo ni zuri kwa kuwa litawezesha wananchi kupata majibu sahihi ya serikali kuliko kusikiliza hoja za upande mmoja.

Walisema hali hiyo pia itasaidia kuondoa dhana potofu kuwa walichokisema wabungewa upinzani bungeni ndicho sahihi.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, alisema hatua ya kujirekodi na kusambaza katika mitandao ya kijamii, mbali na wananchi kupata taarifa sahihi, pia itakuwa fursa ya kisiasa kwa viongozi husika.

“Itatoa nafasi kwa Watanzania ya kujua kila kitu ambacho serikali inakifanya, hivyo ni wazo zuri na linapaswa kuanza kutumika haraka,” alisema Aweso.

Alisema njia hiyo itaiwezesha serikali kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu shughuli mbalimbali inazozitekeleza.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni, alisema niwazo zuri na linafaa kutekelezwa haraka kwa sababu hatua hiyo itaiwezesha serikali kuwapatia taarifa sahihi wananchi na kujitangaza.

Alisema kwa sasa wananchi wamekuwa wakipata taarifa za upande mmoja bila ya majibu ya serikali, hali inayosababisha wananchi kufahamu mabaya ya serikali.

Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, alisema viongozi wa serikali wasiishie kujirekodi tu bali waitumie mitandao ya kijamii kuwapasha habari wananchi katika kila jambo zuri linalifanywa na serikali.

“Majibu yanayotolewa na serikali bungeni ni vizuri yakasambaa kwa wananchi kwa haraka kwa kutumia mitandao ya kijamii, itaiwezesha serikali kujipambanua zaidi kwa wananchi. Mie naona ni wazo zuri na linalopaswa kutekelezwa haraka,” alisema Dk. Mwinyi.

Naye Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, alisemahatua ya kujirekodi kwa mawaziri na kutuma kwenye mitandao ya kijamiiitatoa taswira halisi nini serikali inafanya na inatarajia kufanya nini.

Alisema kutokufanya hivyo kunawafanya wananchi kutokujua serikali yaoinafanya nini na kwamba hatua hiyo itawasaidia pia mawaziri husika kujitangazakatika majimbo yao.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here