SHARE

TIB Corpoate  Bank Limited imeingia ubia na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ili kuunganisha mfumo wa kisasa TAXBANK  utakao tumika katika kukusanya kodi nchini.

Kamishna Jenerali wa TRA Bw.Charles Kichere akikabidhiana mkataba na mkurugenzi mkuu wa TIB Corporate Bank Bw. Frank Nyabundege. Wakishuhudiwa na mkurugenzi wa huduma na elimu kwa wateja wa TRA Bw. Richard Kayombo na Mkuu wa Kitengo na Masoko na mahusiano ya Kampuni wa TIB Corporate Bi. Theresia Soka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es salaam Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Charles Kichere amesema Benki hiyo imejiunga na mfumo huo wa ulipaji kodi ili kusaidia kufanikisha malengo ya Serikali utakaoweza kuongeza ufanisi wa ukusanyaji kodi nchini .

Hata hivyo Kamishna Kichere amesema Benki hiyo imeunganisha mfumo wake wa malipo ya moja kwa moja na mfumo wa TRA ambapo mlipa kodi akilipa katika tawi lolote la Benki taarifa zake zitaonekena mara moja kwenye mtandao wa TRA.

Mkurugenzi mkuu wa TIB Corporate Bank Frank Nyabundege akizungumza juu ya mpango huo

Aidha amesema kupitia mfumo huo mlipa kodi atapata  huduma bora za haraka na kumrahisishia kufanya muamala wa kulipa kodi kwa ufanisi ambapo huduma hiyo itasadia kupunguza makosa mbalimbali ya ulipaji kodi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa TIB Corporate Bank Frank Nyabundege ameahidi kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika kukusanya mapato ili kuinua Uchumi wa Nchi.

 

 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here